Habari za kiuchunguzi tulizodhibitisha kutoka kwa watu wa karibu wa wasanii hao maarufu Wema Sepetu na Diamond Platnumz hawajaachana kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii.
Timu ya wachunguzi wetu kwa takribani wiki nzima ilijichimbia kutafuta chanzo cha kuvunjika kwa uhusiano huo ambao kwa sasa ulikuwa ni uhusiano wenye umaarufu nchini Tanzania na eneo zima la nchi za afrika na pengine hata nje ya mipaka ya afrika kwa wale wanaofutilia habari za wasanii wa Afrika. Umaarufu wao wa wawili hao ulifikia kufananishwa na uhusiano mwingine wa wasanii maarufu duniani hivyi sasa ambao wanafanana sana na wawili, uhusiano wa Kim Kardashian na Msanii wa Muziki maarufu kwa jina Kanye West.
Kwa mujibu wa udhibitisho tuliokusanya unaonyesha kuwa wawili hao "Wapo Pamoja" na kile kinachoendelea kwenye vyombo vya habari ni mipango "iliyopangwa ikapangika" kuonyesha kuvunjika kwa uhusiano huo akizungumza kwa na @mjasiriahabari mmoja wa watu waliokaribu na wawili hao kwa sharti la kutokutajwa jina kwa sababu si msemaji wao amesema "Haya mambo kaka, usisikilize vyombo vya habari Wema na Diamond hawajaachana, chukua maneno yngu utakuja kuniambia baadaye" alisema huku akikataa kufafanua kile anachomaanisha.
Katika kuhakikisha tunapata ukweli wa jambo hilo wachunguzi wetu waliingia ndani zaidi kuwapata watu wa karibu wa wawili hao kwa nyakati tofauti wakiwemo marafiki na jamaa wengine na kudhibitishia @Mjasiriahabari kuwa kile kinachoonekana kwenye vyombo vya habari ni mpango uliopangwa na viongozi wa masuala ya kibiashara wa Diamond ili kutengeneza "biashara" ya video yake mpya aliyozindua siku chache zilizopita, "Kilichofanyika ni kutengeza "PUblicity" ya video yetu mpya, si unajua siku hizi bila vyombo vya habari hakuna kuuza" kilesema chanzo chetu.
Kwa mujibu wa wachambuzi mbalimbali wapo waliokosea "mbinu" hiyo ya kujijengea umaarufu kwa njia hiyo na wako waliounga mkono wakisema ni ubunifu na kukua kwa nguvu ya vyombo vya habari, wadau walienda mbali na kuelezea kuwa aliyebuni mpango huo ni mtu makini na anajua anachokifanya hasa ukizingatia "wimbo mpya wa Diamond umetoka na jina la "Nimpate Wapi" kwa maumbile ya kibinadamu ukiunganisha na tukio la kuvunjika kwa uhusiano wake na Wema Sepetu moja kwa moja itaonekana "Nimpate Wapi mwingine kama Wema" na ndio sababu ilibidi uhusiano uvunjike ili kutngeneza "sensational" jambo ambalo linaonekana kufanikiwa. Wapo ambao wamekwenda mbali wakielezea matukio ya namna hiyo si mara ya kwanza kwa wawili hao kutumia uhusiano wao kujijengea umaarufu wa kazi zao jambo ambalo inasemekana linamnufaisha zaidi Diamond kuliko Wema Sepetu.