Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari mtoto huyo amefanikiwa kujiunga na timu ya Arsenal kwa mkataba rasmi wa miezi sita, ambapo ataendelea kuchezea timu ya watoto ya klabu chini ya miaka 16, na baada ya msimu kumalizika klabu hiyo inatarajia kumpa mkataba rasmi wa ajira ambapo wataalamu na wachambuzi wa masuala husika wanatabiri huwenda ukawa mkataba "mnono" kuwahi kuingia klabu hiyo na mchezaji wa umri mdogo wa miaka 16.
Klabu ya Arsenal inasemekana "imelamba dume" baada ya vilabu vya Chelsea, ManaU navyo kujaribu kutumia ushawishi kumpata kinda huyo lakini haikuwezekana kutokana na kijana huyo mwenyewe kuchagua kubakia Arsenal ambayo alikuwa akifanyia mazoezi yake, ikumbukwe kuwa Baba wa Mtoto huyo, David Beckham hajawahi kuichezea klabu hiyo lakini ana uhusiano mkubwa na Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger na pia alitumia klabu hiyo ya London kufanya mazoezi wakati alipokuwa njiani kujiunga na L A Gallaxy ya Marekani baada ya kuondoka ManU.
Huku habari hizo zikichukuwa "headline" kwenye vyombo vya habari wako wale watakaodhani umaarufu wa baba yake, pamoja na uhusiano wake na klabu ya Arsenal huwenda ndio sababu ya mtoto huyo kupata nafasi hiyo lakini ukweli ni kwamba kijana huyo ameichagua klabu ya Arsenal kwa kuwa na kiwango cha juu cha "Academy" ya soka ulimwenguni na hivyo inaaminika ktk kipindi cha mafunzo yke ktk klabu hiyo atakuwa ameiva kuweza kusajiliwa rasmi.
Wakati huo huo mitandao mbalimbali ya upigaji kura na ubashiri imempa 14/1 kuweza kucheza ligi ya Uingereza #PL na 33/1 kuchezea timu ya taifa ya wakubwa #England.
0 comments:
Post a Comment