Home » » "House Girl" aliyeonekana kwenye Mitandao ya Kijamii akimtesa Mtoto Aishtua Mahakama,

"House Girl" aliyeonekana kwenye Mitandao ya Kijamii akimtesa Mtoto Aishtua Mahakama,

Unknown | 1:22 AM | 0 comments


 Picha ya Bi Jolly Tumuhirwe, ndiye yule "House Girl" picha ya Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha akimtesa na kumpiga mtoto mdogo huku akimlazimisha kula, bint huyu mwenye umri wa miaka 22, kwa mara nyingine tena amewashtua watu waliokuwa mahakamani kwa kukiri kuwa ni kweli alifanya vitendo hivyo dhindi ya mtoto huyo.

Picha ya Mtoto, Naalya, (Mtoto ambaye alifanyiwa vitendo vya kinyama) akiwa pichani pamoja na mama yake Bi Amelia Kamanzi wakiwa mahakamani kusikiliza kesi dhidi ya masaidizi huyo wa nyumbani, mtoto huyo anaonekana kufuatilia, wakati "HouseGirl" huyo akitoa maelezo yke mbele hakimu.
Habari kwa Mujibu wa Mashirika ya habari na Washirika wetu, 
Hivyi karibuni kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ukiwemo mtandao maarufu wa #Wattssap kulisambazwa video ikimwonyesha #HouseGirl mmoja nchini Uganda akimpiaga na kumnyanyasa mtoto wa muajiri wake. Picha za video hiyo ilizua mjadala mkubwa nchini humo jambo lilipelekea Polisi nchini humo kumkamata msaidizi huyo wa nyumbani na kumfikisha mahakamani. Ikiwa ni mara ya pili kufikishwa mahakamani akitokea korokoroni msaidizi huyo wa anayitwa Jolly Tumuhiirwe mwenye umri wa miaka 22 aliwashtua watu waliokuwa mahakamani hapo ikiwemo hakimu anayesikiliza shauri hilo katka mahakama ya mwanzo wilaya ya Wakiso kwa kukiri makosa hayo huku akiwaomba wale wote walioguswa na tukio hilo kumsamehe. Jambo lililozua mshangao mkubwa kwa watu wengi ambao wamekuwa wakihudhuria usikilizaji wa kesi hiyo. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Bw Moses Nahende ilimbidi kuakhirisha kesi hiyo na kupanga tarehe nyingine ya kutoa hukumu ambapo amevitaka vyombo vya upelelezi nchini humo ikiwemo ofisi ya muendesha mashtaka kukamilisha upelelezi wao na kuwasilisha mahakani hapo.
Naye msemaji kutoka ofisi ya muendesha mashtaka mkuu nchini Uganda akizungumza na vyombo vya habari amesema wanachosubiri ni taarifa za upepelezi kutoka polisi ili kuweza kujua ni mashtaka gani watayatumia kuitaka mahakama kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria.
Hapo awali polisi nchini humo walisema mashtaka wanayotarajia kumfungulia mtuhumiwa ni shtaka la kujaribu kuuwa, lengo ikiwa kuitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mhusika ili kuwa fundisho kwa wafanyakazi na wasaidizi wengine wa nyumbani ambao kwa siku za hivyi karibuni kumekuwepo matukio mbalimbali ya wasaidizi wa nyumbani kuwatesa au kuwaua watoto wadogo wanaoachwa nyumbani na wazazi wao kutokana na wazazi hao kuwa na majukumu mbalimbali ya kazi na uzalishaji
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : MJASIRIA HABARI | SALUM ALLY
Copyright © 2013. mjasiriahabari - All Rights Reserved
Template Modify by TheChoiceTz
Designed By TheChoiceTz