Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai akihutubia kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida,
Msindai alikuwa akijitambulisha kuvunja makundi na kupokea kero
mbalimbali za
wananchi.
Baadhi
ya wanaccm na wananchi wa Singida mjini wakimsikiliza kwa makini
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Mgana Izumbe Msindai (hayupo kwenye
picha) wakati akihutubia.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Wanachama
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa mkoa wa Singida kwa
ujumla, wameaswa kutumia mwaka huu mpya, kujiwekea malengo ya
kufanya kazi halali kwa bidii na maarifa ili waweze kujiletea
maendeleo makubwa zaidi kuliko yaliyopatikana mwaka jana.
Changamoto
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Singida Mgana Izumbe Msindai,
wakati akiutubia wananchi wa Manispaa ya Singida kwenye kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo kikuu cha mabasi cha zamani
mjiniSingida.
Amesema
kujituma kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kwa malengo, ndio njia
pekee inayoweza kumsaidia mwananchi ye yote kujikomboa kiuchumi na
kupelekea kuishi maisha bora.
Akifafanua
zaidi, Msindai amesema linapokuja suala la maendeleo, ni lazima itikadi
za kisiasa ziwekwe pembeni, ili maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja,
wilaya, mkoa na hata taifa, yaweze kupatikana.
Msindai
ambaye ni maarufu kwa jina la CRDB benki inayomjali mteja, ametumia
fursa hiyo kuwashukuru wana CCM kwa kumchagua kwa kishindo kushika
nafasi ya mwenyekiti CCM Mkoa.
Wakati
huo huo, Msindai amesema kuwa wamekubaliana na manispaa ya Singida,
kituo kikuu cha zamani cha mabasi, kuanzia sasa kitumike kwa mabasi
madogo kushusha abiria hadi hapo manispaa itakapoanza kujenga kitega
uchumi.
2 comments:
hongera kwa kuwakumbusha wananchi hilo swala
Hongera mjasiriahabari kwa kurejea hewani kwa kishindo tunaamini tutaendelea kufaidi habari na matukio kwa kiwango cha juu!!!!
Post a Comment